Jipime maarifa yako kuhusu ´Aqiydah sahihi
Chemsha Bongo ya ´Aqiydah sahihi 02
15:00
Umemjuaje Mola wako?
- Kwa alama na viumbe Wake
- Kwa kumuota
- Kwa kumtafakari
Ni kipi katika haya ni baadhi ya mfano wa shriki kubwa?
- Kuchinja, kuapa, kusujudu kwa asiye Allaah
- Uongo, kumuua mzazi na liwati kwa dada yako
- Uzinzi, pombe na kumuasi mtawala
Nini malengo ya kuumbwa wanadamu na majini?
- Kula
- Kufanya kazi kwa ajili ya kuiangalia familia yako
- Kumwabudu Allaah
Ni ipi hukumu ya kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?
- Inafaa kama unamuwekea Mtume
- Hapana vibaya kama nia yake ni njema
- Ni shirki kubwa
Je, mtu anakuwa mshirikina kwa kumfanyia ibaadah Mtume au Malaika?
- Hapana, hao ni waja wema
- Ndio, ni mshirikina
- Itategemea na ibaadah gani anamfanyia
Ni dhambi ipi ambayo Allaah haisamehi?
- Kumuua mzazi wako
- Kumzini mama yako
- Shirki kubwa
Ni yepi malipo ya anayekata hirizi kutoka kwa mtu?
- Ni kama ambaye kaacha mtumwa huru
- Atapata tthawabu sawa na mlima wa Uhud
- Ataingia Peponi bila ya hesabu
Nini maana ya ibaadah?
- Ni ile hali ya kumwelekea Allaah katika kila hali
- Ni ile hali ya kumnyenyekea Allaah
- Ni kila anachokipenda na kukiridhia Allaah katika maneno na matendo, yenye kuonekana na yaliyojificha
Ni ipi hukumu ya mwenye kuamini kuwa Qur-aan ni kiumbe?
- Muumini mwenye imani kamili
- Qur-aan ni kiumbe katika viumbe wa Allaah
- Imani hiyo ni ukafiri, kwa.s Qur-aan ni maneno ya Allaah
Ni kipi katika haya ni baadhi ya mfano ya shriki ndogo?
- Mfano wa shirki ndogo ni kusujudia kaburi
- Mfano wa shirki ndogo ni kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah
- Mfano wa shirki ndogo ni kuapa kwa asiyekuwa Allaah
Ni maana ya laa ilaaha illa Allaah?
- Hakuna mungu iila Allaah
- Hakuna mwabudiwa wa haki ila Allaah
- Hakuna mwenye kuhukumu ila Allaah
Je, kuna uwezekano mshirikina akaingia Peponi?
- Ndio, kama ametenda mema mengi
- Ndio, Allaah anaweza kumwingiza kwa rehema Yake
- Hapana, Pepo ni haramu kwa mshirikina na kafiri
Ni nini maana ya Mola?
- Yule Mkuu
- Mkubwa kuliko kila kitu
- Mmiliki na mwabudiwa
Ni ipi hukumu ya mwenye kufa juu ya shirki kubwa?
- Anaweza kusamehewa kama ana mema yake yatazidi mabaya
- Allaah ataamua cha kumfanya
- Ni kafiri na atakaa Motoni milele
Ni ipi hukumu ya matabano (Ruqyah)?
- Matabano hayafai na ni shirki
- Matabano ya Qur-aan, Sunnah na dawa zinazokubalika yanafaa
- Anayefanya matabano hamtegemei Allaah
Ni ipi hukumu ya mwenye kusema Allaah yuko kila mahali?
- Ni sahihi
- Ni ukafiri kama anakusudia yuko kila mahali kwa dhati Yake
- Kufanya hivo ndio upwekeshaji
Ni aina ipi kubwa kabisa ya ibaadah?
- Du'aa
- Kuwapiga jihaad maadui wa Allaah
- Swalah tano
Ni ipi katika haya ni tofauti ya shirki kubwa na ndogo?
- Shirki ndogo inaharibu matendo yote kinyume na shirki kubwa
- Shirki ndogo inamtia mwenye nayo milele Motoni kinyume na shirki kubwa
- Shirki kubwa inamtia mwenye nayo milele Motoni kinyume na shirki ndogo
Anakuwa mpwekeshaji mtu anayempwekesha Allaah katika matendo Yake lakini akamshirikisha katika ‘ibaadah Zake?
- Hapana, lazima ampwekeshe katika ´ibaadah
- Ndio, kwa.s amefanya aina mojawapo ya Tawhiyd
- Ni mpwekeshaji maadamu anaswali swalah tano
Ni ipi hukumu ya kutundika na kuvaa hirizi ya Aayah za Qur-aan?
- Hirizi ya Qur-aan inafaa
- Sahihi ni kwamba haifai
- Inafaa tu kama anaivaa juu ya mavazi safi
Ni ipi hukumu ya kuapa kwa Mtume?
- Haifai na ni shirki kubwa
- Inafaa tu kuapa kwa Ka'bah
- Ni dhambi ya kawaida
Ukifungua mwanzo wa msahafu ni ipi amri ya kwanza aliyoamrisha Allaah?
- Kuswali vipindi vitano
- Kuwafanyia wema wazazi
- Kumwabudu Allaah na kutomfanyia washirika na wenza