Jipime maarifa yako kuhusu siku na swalah ya idi
Chemsha Bongo siku na swalah ya idi 04
09:10
Je, kunaswaliwa swalah ya mamkizi ya msikiti kabla ya swalah ya idi?
- Hakuna kwa hali yoyote
- Ndio, inaposwaliwa msikitini tu
- Ni Bid'ah
Ni kwanini inapendeza kuchelewesha swalah ya idi?
- Ili watu wapate muda wa kutosha wa kutoa Zakaat-ul-Fitwr
- Ili watu wapate muda mzuri wa kulala
- Ili watu wapate muda wa kutayarisha vyakula aina mbalimbali
Je, inafaa kuzungumza katika Khutbah za idi mbili?
- Hapana, ni dhambi
- Ndio, inafaa
- Hapana, hana swalah
Ambaye hajakamilisha swawm ya Ramadhaan akifunga siku sita za Shawwaal anapata malipo ya kufunga mwaka mzima?
- Hapana, ni bure
- Si lazima akamilishe anaweza kuanza
- Anaweza kupata, lakini salama na bora zaidi kukamilisha kwanza Ramadhaan kisha ndio uanze Shawwaal
Takbiyr za swalah ya idi Fitwr Rakah ya pili ni ngapi?
- Ni 4 baada baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam
- Ni 5 baada ya Takbiyr al-Intiqaal
- Ni 7 baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam
Ni sikukuu zipi ambazo waislamu wanatakiwa kusherehekea?
- Siku ya mama na siku ya ijumaa
- maulidi na mwaka mpya wa kiislamu
- Idi al-Fitwr na idi al-Adhwhaa
Mtu akikosa swalah ya idi anaruhusiwa kuikidhi?
- Hapana, hakuna namna
- Ndio, kwa sifa yake
- Ataiswali kama Dhuhr
Ni kipi kilichosihi katika haya?
- Ni lazima mtu aswali zote mbili la sivyo anapata dhambi
- Ni wajibu kwa imamu tu
- Ni lazima kuswali mojawapo na si lazima kuswali zote isipokuwa kwa imamu tu
Ni lini wakati bora wa kutekeleza Sunnah ya kuoga kwa ajili ya idi?
- Kufurahi na kumshukuru Allaah kwa kumaliza mfungo wa Ramadhaan
- Kula na kunywa baada ya mfungo
- Familia kukutana na kusalimiana
Je, imesuniwa kwa imamu kunyanyua mikono wakati wa Takbiyr za swalah?
- Hapana, hiyo ni Bid'ah
- Ndio, Sunnah kwa maamuma tu
- Ndio, ni Sunnah kwa imamu na maimamu
Je, inafaa kwa ambaye amekosa swalah ya idi kuikidhi mwenyewe au na familia yake?
- Wanazuoni wengi wanaona kuwa inafaa
- Haifai ni Bid´ah
- Inafaa tu kama ni swalah ya idi al-Fitwr na si idi al-Adhwhaa