Jipime maarifa yako kuhusu siku na swalah ya idi
Chemsha Bongo siku na swalah ya idi 03
09:10
Je, inafaa kwa waislamu kupeana zawadi kwa ajili ya idi?
- Ndio, ni katika furaha ya kishari'ah
- Hapana, ni kujifananisha na makafiri
- Ndio, ila kwa watoto tu
Ni Sunnah kuleta Takbiyr ya idi baada ya zile swalah za faradhi tano?
- Hapana, ni Bid'ah
- Ni Sunnah kwa wale wanaoswali mkusanyiko na si wanaoswali peke yao
- Ni Bid'ah potofu
Sherehe ya idi Adhwhaa ni siku ngapi?
- Siku saba
- Siku ya moja
- Siku tatu
Lini ni sawa kuswali swalah ya idi msikitini?
- Wakati wa jua kali
- Wakati wa dharurah kama mvua
- Wakati imamu ataamua kufanya hivo
Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya idi?
- Haramu
- Ni Sunnah
- Ni Sunnah inayokokoteza
Khutbah ya idi ni moja au mbili?
- Moja, ijapo wako wenye kuona ni mbili
- Khutbah moja tu ni Bid'ah
- Mwenye kusema ni Khutbah mbili ni mpotevu
Ni kipi kilichosihi katika haya?
- Karibu na kutaka kutoka kwenda kuswali idi
- Usiku wa kuamkia idi
- Wakati wowote tu muhimu mtu aoge
Ni lini wakati bora wa kutekeleza Sunnah ya kuoga kwa ajili ya idi?
- Karibu na kutaka kutoka kwenda kuswali idi
- Usiku wa kuamkia idi
- Wakati wowote tu muhimu mtu aoge
Ni ipi hukumu ya zile Takbiyr 7 katika ile Rakah ya kwanza na Takbiyr 5 katika ile Rakah ya pili?
- Ni wajibu kuzileta la sivyo swalah haisihi
- Ni Sunnah ya kutosheleza
- Zinapendeza na zinadondoka kwa kusahau
Ni ipi Sunnah kwa wakazi wa Makkah juu ya swalah ya idi?
- Kuswali kwenye msikiti wao Mtakatifu
- Kutoka kwenda kuswali uwanjani au jangwani
- Kutoka kwenda kuswali uwanjani
Ni ipi Sunnah kwa wakazi wa Madiynah juu ya swalah ya idi?
- Kutoka kwenda kuswali uwanjaji na jangwani
- Kuswali kwenye msikiti wa Qubaa
- Kuswali kwenye msikiti wa Qiblatayn