Jipime maarifa yako kuhusu Manhaj
Chemsha Bongo masuala ya Manhaj 02
15:00
Ni kipi sahihi katika haya?
- Jamaa´at-ut-Tabliygh ni katika Ahl-us-Sunnah
- Jamaa´at-ut-Tabliygh ni katika Suufiyyah
- Jamaa´at-ut-Tabliygh ni katika Jahmiyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa imani ni kukubali kwa ulimi na kusadikisha kwa moyo?
- Jahmiyyah
- Maaturiydiyyah
- Qadariyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa imani ni kuamini na kusadikisha moyoni peke yake?
- Khawaarij
- Ashaa'irah
- Jabriyyah
Ni kipi sahihi katika haya?
- Muislamu mtenda dhambi kubwa ni kafiri
- Muislamu mtenda dhambi kubwa ni muumini
- Muislamu mtenda dhambi kubwa ni muumini mwenye imani pungufu
Ni sifa zipi tatu muhimu ambazo zinawatofautisha Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Bid’ah?
- Kulingana juu ya 'Arshi, kuzungumza na kuja
- Allaah kuwa juu, kuzungumza na kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah
- Allaah kuwa juu, kuonekana na mkono wa Allaah
Ni imamu yupi katika hawa ambaye alisema (Kulingana juu kunafahamika na namna haifahamiki) yanayotumika kama kanuni katika sifa zote za Allaah?
- ash-Shaafi'iy
- Abu Haniyfah
- Maalik
Tofauti iliopo ya maana ya imani kati ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaaah na wanazuoni wa Murji-ah al-Fuqahaa ni ya kimaana tu au ya kihakika?
- Sahihi ni kwamba ni ya kihakika
- Ni ya kimaana na si ya kihakika
- Hakuna tofauti yoyote kati yao
Ni lipi katika makundi haya potofu linalosema kuwa Jibriyl ameichukua Qur-aan kutoka kwenye Ubao uliohifadhiwa au kwamba Allaah aliiumba kwenye kitu ambapo Jibriyl akaichukua kutoka katika kitu hicho?
- Jabriyyah
- Jahmiyyah
- Murji-ah
Ni sahihi kufasiri laa ilaaha illa Allaah kwamba maana yake ni hakuna mwenye kuhukumu isipokuwa Allaah?
- Si sahihi, ni tafsiri ya kizushi
- Ni sahihi kabisa ndio malengo ya shahaadah
- Ni sahihi na asiyefasiri hivo siyo mpwekeshaji
Ni kipi sahihi katika haya?
- Imani za watu zinatofautiana na kushindana
- Imani za watu zinalingana
- Imani ni kitu kimoja kisichogawanyika
Ni kipi sahihi katika haya?
- Qur-aan ni maneno ya Allaah, sawa herufi na maana yake
- Qur-aan ni maneno ya Allaah herufo na si maana yake
- Qur-aan si maneno ya Allaah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa Qur-aan ni ibara ya maneno ya Allaah?
- Maaturiydiyyah
- Raafidhwah
- Ashaa'irah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalopinga kuonekana kwa Allaah kabisa na kwamba haiyumkiniki?
- Suufiyyah
- Jahmiyyah
- Murji-ah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa Allaah anaonekana duniani na Akhera?
- Suufiyyah
- Jahmiyyah
- Shiy'ah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa Shahaadah maana yake ni kuondosha yakini mbovu na kuingiza yakini sahihi juu ya Allaah?
- al-Ikhwaan al-Muslimuun
- Jamaa'at-ut-Tabliygh
- Khawaarij
Ni kipi sahihi katika haya?
- Qaadiyaaniyyah ni waislamu waliokosea
- Qaadiyaaniyyah ni makafiri
- ´Aqiydah ya Qaadiyaaniyyah ni sahihi
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa imani ni kutamka kwa ulimi peke yake?
- Ashaa'irah
- Karraamiyyah
- Khawaarij
Je, mtu anaweza kuwa muumini akiacha matendo yote kabisa bila udhuru?
- Ndio, inawezekana
- Hapana, haiwezekani
- Ni muumini kwa kiasi cha matendo aliyoacha
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa Qur-aan ni simbulizi (hikaya) ya maneno ya Allaah?
- Maaturiydiyyah
- Mu'tazilah
- Murji-ah
Ni sifa ngapi za Allaah wanazothibitisha Ashaairah?
- 20
- 7
- 15
Ni nani katika makafiri hawa aliyesema kuwa Qur-aan si maneno ya Allaah?
- Fir'awn
- Waliyd bin al-Mughiyrah
- Abu Lahab
Ni nani mwanzishi wa Jamaa´at-ut-Tabliygh?
- Jamh bin Swafwaan
- Muhammad bin Ilyaas
- Muhammad Ayyuub