Jipime maarifa yako kuhusu Manhaj
Chemsha Bongo masuala ya Manhaj
15:00
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa waumini hawatomuona Allaah siku ya Qiyaamah?
- Ahl-us-Sunnah
- Ashaa'irah
- Jahmiyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linaloamini kuwa Qur-aan ni kiumbe na si maneno ya Allaah?
- Ashaa'irah
- Jahmiyyah
- Qadariyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa imani ya Jibriyl na Khawaarij inalingana na imani ya mtenda maovu mkubwa zaidi katika viumbe?
- Khawaarij
- Murji-ah
- Qadariyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalopinga makadirio (Qadar)?
- Qadariyyah
- Khawaarij
- Mu'tazilah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalothibitisha majina ya Allaah na kukanusha sifa Zake?
- Mu'tazilah
- Jahmiyyah
- Qadariyyah
Murji-ah al-Fuqahaa’ ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaaah?
- Ndio
- Hapana
- Ni wazushi wa kupindukia
Ni wapi wametofautiana Khawaarij na Ahl-us-Sunnah inapokuja katika suala la imani?
- Khawaarij wanaona kuwa haizidi wala haipungui
- Khawaarij wanaona kuwa inazidi lakini haipungui
- Khawaarij wanaona kuwa haipungui lakini inazidi
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa waumini watamuona Allaah lakini si kutoka upande wowote?
- Jahmiyyah
- Khawaarij
- Ashaa'irah
Ni kipi katika haya ni imani ya Murji-ah al-Fuqahaa waliyokosea katika suala la imani?
- Hawaoni kuwa imani inazidi wala kupungua
- Wanamkufurisha mtenda dhambi kubwa
- Wanaona kuwa imani inazidi na kupungua, lakini matendo si sehemu katika imani
Ni kundi potofu lipi katika haya linalopinga adhabu ya ndani ya kaburi?
- Maaturiydiyyah
- Mu'tazilah
- Jabriyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa mja ametenzwa nguvu katika matendo yake na kwamba hana khiyari?
- Jahmiyyah
- Jabriyyah
- Khawaarij
Ni kundi potofu lipi katika haya linaloona kuwa matendo si katika imani?
- Murji-ah
- Khawaarij
- Raafidhwah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa Qur-aan ni maana iliyo ndani ya nafsi ya Allaah?
- Murji-ah
- Ashaa'irah
- Raafidhwah
Ni kundi potofu lipi katika haya muuminl mwenye kufa katika dhambi kubwa si muumini wala si kafiri, yuko katika ngazi kati ya ngazi mbili?
- Khawaarij
- Mu'tazilah
- Murji-ah
Ni nani mwanzilishi wa kikundi cha Jahmiyyah?
- Ubayy bin Saluul
- Jahm bin Swafwaan
- Amr bin 'Ubayd
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa Maswahabah wote ni makafiri isipokuwa 7-8 tu?
- Qadariyyah
- Raafidhwah (Shiy'ah)
- Jabriyyah
Ni kina nani katika hawa wanaopinga na kukataa majina na sifa za Allaah?
- Khawaarij
- Qadariyyah
- Jahmiyyah
Ni sentesi ipi katika hizi ni sahihi?
- Imani ni maneno na matendo
- Imani inazidi lakini haipungui
- Imani ni kutamka pekee bila kufanya matendo
Hii leo wapo wale Qadariyyah wanaosema kuwa Allaah hayajui mambo ya viumbe Wake isipokuwa baada ya kutokea?
- Wapo tena wengi
- Hakuna, walikuwepo zamani
- Wapo kati ya Jahmiyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa imani ni kule kutambua ndani ya moyo peke yake?
- Jahmiyyah
- Ashaa'irah
- Qadariyyah
Ni kundi potofu lipi katika haya linalosema kuwa muumini mwenye kufanya dhambi kubwa ni kafiri?
- Ashaa'irah
- Khawaarij
- Shiy'ah
Ni nani mwanzilishi wa Mu’tazilah?
- Amr bin 'Ubayd
- Jahm bin Swafwaan
- Bishr al-Mariysiy