Swali: Nina mwana anayetamani kuoa, lakini haswali na anafanya baadhi ya maasi. Ninataka kumuozesha huenda hilo likawa sababu ya kurekebika kwa maisha yake. Je, inajuzu kufanya hivyo? Una nasaha gani?
Jibu: Ni wajibu wako kumpa nasaha na kumtia adabu mpaka aanze kuswali. Haikufai kumuozesha mpaka aswali, kwa sababu kuacha swalah ni ukafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Baina ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”[1]
“Ahadi iliyopo kati yetu na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”[2]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atuongoze sisi na yeye na tunamuomba akupe msaada katika kumrekebisha. Katika sababu za kumrekebisha ni kumtahadharisha na marafiki wabaya na kumuelekeza kukaa na watu wema. Tunamuomba Allaah akusaidie na amsaidie katika kila lenye kheri na usahihi wa hali yake.
[1] Muslim (82).
[2] at-Tirmidhiy (2621).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/73)
- Imechapishwa: 19/03/2026
Swali: Nina mwana anayetamani kuoa, lakini haswali na anafanya baadhi ya maasi. Ninataka kumuozesha huenda hilo likawa sababu ya kurekebika kwa maisha yake. Je, inajuzu kufanya hivyo? Una nasaha gani?
Jibu: Ni wajibu wako kumpa nasaha na kumtia adabu mpaka aanze kuswali. Haikufai kumuozesha mpaka aswali, kwa sababu kuacha swalah ni ukafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Baina ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”[1]
“Ahadi iliyopo kati yetu na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”[2]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atuongoze sisi na yeye na tunamuomba akupe msaada katika kumrekebisha. Katika sababu za kumrekebisha ni kumtahadharisha na marafiki wabaya na kumuelekeza kukaa na watu wema. Tunamuomba Allaah akusaidie na amsaidie katika kila lenye kheri na usahihi wa hali yake.
[1] Muslim (82).
[2] at-Tirmidhiy (2621).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/73)
Imechapishwa: 19/03/2026
https://firqatunnajia.com/posa-ya-mwanaume-asiyeswali/