Swali: Vipi kuhusu anayethibitisha kuwa Allaah anazungumza pale anapotaka lakini akasema kuwa Qur-aan si kutoka kwenye Ubao uliohifadhiwa?

Jibu: Hapana kizuizi. Allaah amezungumza kwa Qur-aan na kaandikwa katika Ubao uliohifadhiwa. Yote mawili ni sahihi. Allaah amezungumza kwayo na imehifadhiwa katika Ubao uliohifadhiwa, kama ilivyohifadhiwa ndani ya vifua na ndani ya misahafu sasa. Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoteremshwa na si kiumbe, yaliyoandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, yamehifadhiwa ndani ya vifua na yamehifadhiwa katika misahafu. Popote inaposomeka ni maneno ya Allaah, popote inapohifadhiwa ni maneno ya Allaah, popote ilipoandikwa ni maneno ya Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31115/حكم-القول-بان-القران-نزل-من-اللوح-المحفوظ
  • Imechapishwa: 03/10/2025