Pongezi njema za mwaka mpya wa Kiislamu

Swali: Kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Kiislamu imekuwa ni jambo la kawaida watu kukumbushana juu ya kutubia na kuomba msamaha pamoja na kupongezana juu ya ujio wa mwaka mpya…

Jibu: Yote haya ni uzushi. Hakuna mwaka mpya. Hiki ni kitu cha kiistilahi tu. Wakati wowote uhai wako unaweza kumalizika, mwezi wowote, wiki yoyote, siku yoyote – kutegemea siku ya kuzaliwa kwako. Si jambo linalotakiwa kufungamanishwa na Muharram peke yake. Hiki ni kitu cha kiistilahi tu.

Wakati ´Umar alipokuwa anapokea barua ambazo hazina tarehe na wala hajui zimeandikwa wakati gani, ndipo akawataka ushauri Maswahabah. Ni kweli kwamba kalenda ya gregori ilikuweko, lakini hakuwa wanataka kuwaigiliza mayahudi na manaswara. Ndipo wakaafikiana kutokea kwa kuanzia pale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipohajiri, kwa sababu ndio ilikuwa tukio kubwa katika Uislamu. Kwa hivyo wakafanya ndio matokeo ya kalenda ya Kiislamu kutokana na manufaa na haja. Kwa hiyo mwaka mpya wa Kiislamu hautakiwi kufanywa maalum kwa kupeana hongera wala du´aa. Kwa sababu hakuna dalili ya hilo na hivyo jambo hilo inakuwa Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 02/05/2021