Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
”Hatukutuma kabla yako isipokuwa ni wanaume Tunawafunulia Wahy, hivyo basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.”[1]
Ni lazima kwa mwanafunzi kuwauliza wanazuoni na kuthibitisha kwa wanazuoni. Pengine akatahiniwa na mtu ambaye anafikiri kuwa ni katika wanazuoni ilihali ukweli wa mambo ni katika wapotevu na katika watu wa dunia. Pindi watu walipowapa mgongo wanazuoni wao na wakaanza kurejea katika watu wasiostahiki, ndipo waislamu wakazidi kuangamia zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah hatoiondoa elimu hii kwa kuinyakua kutoka kwenye vifua vya wanachuoni, lakini ataiondoa elimu kwa kufa kwa wanachuoni, mpaka pasibakie mwanachuoni yoyote ndipo watu watawachukua viongozi wajinga. Watawauliza maswali wafutu bila ya elimu. Matokeo yake watapotea na kuwapoteza wengine.”[2]
Hatuwataki jamii nzima wote wawe wanazuoni, lakini tunachowataka ni wao kuwaigiliza wanazuoni na kuwauliza wanazuoni. Hii leo fitina zimekuwa nyingi na propaganda zinazoifanya haki kuonekana kuwa ni batili na batili kuonekana kuwa ni haki. Kwa ajili hiyo ni lazima kwa waislamu kurejea kwa wanazuoni wao na kuwauliza kuhusu mambo yanayowazunguka.
[1] 16:43
[2] al-Bukhaariy (100).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 225-226
- Imechapishwa: 31/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket