Swali: Ni jambo limeenea siku hizi picha za sanamu juu ya baadhi ya majengo. Miongoni mwazo ni picha ya simba katika nembo ya saa za Orient, kaskazini mwa msikiti huu na mengineyo. Je, ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haijuzu kuchukua picha, si za wanyama wa mifugo wala za wanaadamu, si juu ya nyumba wala juu ya visivyo nyumba, kama milango na yanayofanana na milango. Bali ni wajibu kukataza jambo hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Usiache picha yoyote isipokuwa uifute.”

Amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) picha katika nyumba au kuzitengeneza. Kwa hiyo haijuzu kuning’iniza picha juu ya kuta, si sanamu wala zisizo sanamu. Ni wajibu kukataza jambo hili. Vilevile ni lazima kuwafikishia watawala jambo hili la maovu. Ni lazima kuwafikishia watawala na tujitegemee katika kuondoa jambo hili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1483/حكم-الصور-المجسمة-من-الحيوانات
  • Imechapishwa: 21/12/2025