Swali: Je, picha zinazorushwa moja kwa moja zinaingia katika zile picha za haramu?

Jibu: Ndio, ni kipi kinachozitoa? Zote ni picha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Hili ni lenye kuenea. Yule anayebagua aina fulani ya picha alete dalili. Lakini hata hivyo kunaruhusiwa zile picha kwa ajili ya dharurah. Haina neno, ikiwa ni kwa ajili ya dharurah:

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

”Kwani mna nini hata msile katika vile ambavyo vimetajiwa jina la Allaah na ilihali ameshapambanua kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura.”[1]?

Ikiwa kuna dharurah inafaa. Lakini bila ya dharurah, kama kwa ajili ya burudani, kuzitazama na kumbukumbu, hazijuzu.

[1] 06:119

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (45)
  • Imechapishwa: 25/07/2024