Swali: Vipi ikiwa ni katika kujenga misikiti?
Jibu: Hapana, misikiti haijengwi kwa zakaah. Misikiti na shule hazijengwi kwa zakaah, bali hujengwa kwa misaada ya watu wa kheri. Ama zakaah hutolewa katika yale aliyoyataja Allaah (´Azza wa Jall):
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيل
“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa].”[1]
Katika njia ya Allaah ni wapigana jihaad kwa mujibu wa wanazuoni.
[1] 09:60
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1708/حكم-بناء-المساجد-من-الزكاة
- Imechapishwa: 06/06/2026
Swali: Vipi ikiwa ni katika kujenga misikiti?
Jibu: Hapana, misikiti haijengwi kwa zakaah. Misikiti na shule hazijengwi kwa zakaah, bali hujengwa kwa misaada ya watu wa kheri. Ama zakaah hutolewa katika yale aliyoyataja Allaah (´Azza wa Jall):
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيل
“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa].”[1]
Katika njia ya Allaah ni wapigana jihaad kwa mujibu wa wanazuoni.
[1] 09:60
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1708/حكم-بناء-المساجد-من-الزكاة
Imechapishwa: 06/06/2026
https://firqatunnajia.com/pesa-ya-zakaah-haijengewi-misikiti/