Katika hali hii jengo linatolewa zakaah ya kodi na ya thamani yake

Swali: Ikiwa mtu ana jengo analolipangisha kwa kodi ya kila mwaka – je, atoe zakaah katika mapato yake au katika thamani ya jengo lenyewe?

Jibu: Ikiwa analitumia kwa upangishaji wala halijawekwa kwa ajili ya kuuza, basi anatoa zakaah katika mapato ya kodi. Ama ikiwa amelinuia kwa biashara au amelihesabu kuwa ni la biashara, hali analipangisha, nalo likiwa limeandaliwa kwa biashara, basi atatoa zakaah kwa vyote viwili: atatoa zakaah ya kodi na atatoa zakaah ya thamani ya jengo kila mwaka. Ama ikiwa limeandaliwa kwa ajili ya upangishaji tu, hakulinuia kwa kuuza, basi atatoa zakaah ya mapato yake pale yanapokamilisha mwaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1690/كيفية-اخراج-زكاة-من-له-عمارة-مستغلة-للايجار
  • Imechapishwa: 06/06/2026