Swali: Wakati wa swalah mtu amesahau kusoma al-Faatihah au amekosa baadhi ya Tasbiyh. Ni ipi hukumu ya swalah yake?
Jibu: Ikiwa atasahau al-Faatihah anapaswa kurudia swalah, kwa sababu al-Faatihah ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah. Ikiwa alikuwa ni imamu au anaswali peke yake na hakusoma al-Faatihah, basi swalah yake haisihi. Ikiwa alisahau katika Rak´ah ya kwanza, basi Rak´ah ya pili inachukua nafasi yake. Vivyo hivyo ataleta Rak´ah badala ya ile aliyosahau kusoma al-Faatihah na walioko nyuma yake wanapaswa kumnasihi na kumkumbusha anaposahau.
Kuhusu maamuma akiacha kwa kusahau, basi tunatarajia hilo linamtosheleza, kwa sababu jopo la wanazuoni wengi wanaona kuwa kisomo cha imamu kinamtosheleza maamuma. Lakini asiiache kwa makusudi. Ni wajibu kwake kusoma al-Faatihah na wala asiiache kwa makusudi. Lakini akiisahau na akamfuata anayesema kuwa halimlazimu maamuma au akaamini kuwa halimlazimu maamuma, basi swalah yake ni sahihi. Ama imamu na anayeswali peke yake hawana udhuru katika hilo. Ni wajibu wao ni kuisoma. Akiisahau katika Rak´ah moja, basi Rak´ah nyingine inachukua nafasi yake, kisha analeta Rak´ah nyingine badala yake.
Swali: Je, atasujudu sujudu ya kusahau?
Jibu: Atasujudu sujudu ya kusahau, ndiyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1717/حكم-نسيان-قراءة-الفاتحة-في-الصلاة
- Imechapishwa: 06/06/2026
Swali: Wakati wa swalah mtu amesahau kusoma al-Faatihah au amekosa baadhi ya Tasbiyh. Ni ipi hukumu ya swalah yake?
Jibu: Ikiwa atasahau al-Faatihah anapaswa kurudia swalah, kwa sababu al-Faatihah ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah. Ikiwa alikuwa ni imamu au anaswali peke yake na hakusoma al-Faatihah, basi swalah yake haisihi. Ikiwa alisahau katika Rak´ah ya kwanza, basi Rak´ah ya pili inachukua nafasi yake. Vivyo hivyo ataleta Rak´ah badala ya ile aliyosahau kusoma al-Faatihah na walioko nyuma yake wanapaswa kumnasihi na kumkumbusha anaposahau.
Kuhusu maamuma akiacha kwa kusahau, basi tunatarajia hilo linamtosheleza, kwa sababu jopo la wanazuoni wengi wanaona kuwa kisomo cha imamu kinamtosheleza maamuma. Lakini asiiache kwa makusudi. Ni wajibu kwake kusoma al-Faatihah na wala asiiache kwa makusudi. Lakini akiisahau na akamfuata anayesema kuwa halimlazimu maamuma au akaamini kuwa halimlazimu maamuma, basi swalah yake ni sahihi. Ama imamu na anayeswali peke yake hawana udhuru katika hilo. Ni wajibu wao ni kuisoma. Akiisahau katika Rak´ah moja, basi Rak´ah nyingine inachukua nafasi yake, kisha analeta Rak´ah nyingine badala yake.
Swali: Je, atasujudu sujudu ya kusahau?
Jibu: Atasujudu sujudu ya kusahau, ndiyo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1717/حكم-نسيان-قراءة-الفاتحة-في-الصلاة
Imechapishwa: 06/06/2026
https://firqatunnajia.com/mswaliji-amesahau-kusoma-al-faatihah/