Swali: Ni ipi hukumu ya kurusha vijiwe siku ya tatu vyote kwa pamoja na akavipanga kwa nia?
Jibu: Ikiwa mtu atachelewesha kurusha vijiwe katika Hajj mpaka akayarusha siku ya kumi na mbili kwa mpangilio, akaanza na kiguzo cha ´Aqabah ya siku ya kumi na moja, akarusha saba kwa kila kiguzo, kisha akarusha ya siku ya kumi na mbili, kisha ya siku ya kumi na tatu kwa nia, basi hilo halina tatizo wala haina ubaya. Lakini amekosa fadhilah na amekosa Sunnah. Sunnah ni kurusha vijiwe kweye kiguzo katika wakati wake, ya siku ya ´Iyd katika wakati wake, ya siku ya kumi na moja katika wakati wake na ya siku ya kumi na mbili katika wakati wake. Hata hivyo kama kulikuwa na sababu ya msongamano, hakuweza au aliogopa nafsi yake na hivyo akaahirisha na akarusha siku ya kumi na tatu au siku ya kumi na mbili kwa mpangilio, basi hilo linamtosheleza.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1714/ما-حكم-الرمي-في-اليوم-الثالث-جميع-الحصيات-ويرتبها-بنية
- Imechapishwa: 06/06/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kurusha vijiwe siku ya tatu vyote kwa pamoja na akavipanga kwa nia?
Jibu: Ikiwa mtu atachelewesha kurusha vijiwe katika Hajj mpaka akayarusha siku ya kumi na mbili kwa mpangilio, akaanza na kiguzo cha ´Aqabah ya siku ya kumi na moja, akarusha saba kwa kila kiguzo, kisha akarusha ya siku ya kumi na mbili, kisha ya siku ya kumi na tatu kwa nia, basi hilo halina tatizo wala haina ubaya. Lakini amekosa fadhilah na amekosa Sunnah. Sunnah ni kurusha vijiwe kweye kiguzo katika wakati wake, ya siku ya ´Iyd katika wakati wake, ya siku ya kumi na moja katika wakati wake na ya siku ya kumi na mbili katika wakati wake. Hata hivyo kama kulikuwa na sababu ya msongamano, hakuweza au aliogopa nafsi yake na hivyo akaahirisha na akarusha siku ya kumi na tatu au siku ya kumi na mbili kwa mpangilio, basi hilo linamtosheleza.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1714/ما-حكم-الرمي-في-اليوم-الثالث-جميع-الحصيات-ويرتبها-بنية
Imechapishwa: 06/06/2026
https://firqatunnajia.com/amerusha-vijiwe-vyote-kwa-pamoja-siku-ya-tatu-kwa-manuizi/