Swali: Ni ipi hukumu ya sigara na shisha? Ni ipi dalili ya kuharamishwa kwake ilihali havimpotezei mtu akili?

Jibu: Ilitangulia katika darsa iliyopita kuwa shisha na sigara vyote viwili ni haramu. Vina madhara mengi. Huenda vikamfanya mtumiaji wake apate kizunguzungu akivitumia baada ya muda mrefu, anaweza kupata kizunguzungu na akaanguka kutoka juu ya mnyama wake au katika hali nyingine pamoja na madhara yake mengi. Ndani yake kuna madhara makubwa yaliyoamuliwa na madaktari. Vinamdhuru mtu katika mwili wake, katika kifua chake na katika mambo mengine. Vina madhara mengi. Kwa sababu hiyo basi ni miongoni mwa vilivyoharamishwa. Hairuhusiwi kuvitumia, wala kuviuza, wala kuvinunua na wala kuviingiza kutoka nje.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1723/حكم-الدخان-والشيشة
  • Imechapishwa: 06/06/2026