Pepo kwa yule anayejishughulisha na makosa yake

Swali: Ni upi sahihi wa Hadiyth ya Anas:

”Pepo (طوبى) kwa yule ambaye anajishughulisha na makosa yake badala ya makosa ya wengine.”?

Jibu: Haina neno. Ni nzuri kwa mujibu wa Haafidhw [Ibn Hajar] (Rahimahu Allaah).

Swali: Inakuweje pale mtu anapotaja kasoro za watu kwa lengo la kutahadharisha?

Jibu: Ikiwa ataangalia kasoro za watu azitahadharishe. Azitafakari ili azitahadharishe. Makosa za watu katika ghadhabu, makosa ya watu katika haraka, makosa ya watu katika usengenyi. Anatakiwa kuzingatia yale maovu yanayotokana nayo ili aweze kuyatahadharisha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25222/هل-صح-حديث-من-شغله-عيبه-عن-عيوب-الناس
  • Imechapishwa: 18/02/2025