Swali: Una nasaha gani kwa anayekata tamaa juu ya yale Ummah wa Kiislamu uliyofikia na yale Ahl-ul-Ahwaa´ waliyofikia katika njia za mawasiliano?

Jibu: Haijuzu. Kukata tamaa haijuzu:

إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ

“Hakika hawakati tamaa na faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri.” (12:87)

وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ

“Na nani anayekata tamaa na rehema za Mola wake isipokuwa waliopotea.” (15:56)

Hatutakiwi kukata tamaa na kuacha kujaribu kuondosha shari. Hatutoiacha. Bali tunatakiwa kujaribu na kufanya kile tunachoweza. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko pamoja na sisi ikiwa tutakuwa wakweli. Haijuzu kuvunjika moyo na kukata tamaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–14330804.mp3