Pale ambapo Hadiyth zinatofautiana

Swali: Ni vipi kukusanya kati ya Hadiyth zenye kutofautiana?

Jibu: Udhahiri ni kwamba inatokana na hifdhi ya wale wasimulizi. Kanuni inasema kwamba mwenye kuzidisha inakubaliwa ziada yake. Hivo ndivo kanuni inavosema. Wakizidishiana basi ile ziada inakubaliwa muda wa kuwa yule mzidishaji ni mwaminifu. Vivyo hivyo ndivo inavokuwa juu ya yale maongezi ya watu hii leo. Kanuni inasema kuwa nyongeza inakubaliwa inaposimuliwa na mwaminifu.

Swali: Vipi ikiwa yule ambaye hakusimulia ziada ndiye madhubuti zaidi?

Jibu: Haijalishi kitu. Haidhuru muda wa kuwa ziada hiyo haiendi kinyume. Haafidhw Ibn Hajar amesema katika “an-Nukhbah”:

“Ziada ya mbili hizo – yaani Swahiyh na nzuri – ni yenye kukubaliwa.”

Hapa ni pale ambapo haipingani na ambaye ni madhubuti zaidi. Kwa sharti hayapingani. Msimulizi mmoja amesema 100 na mwengine amesema 120. Katika hali hii hakuna mgongano. Kilichopo ni kwamba yule msimulizi wa 100 amepitwa na hakutambua hiyo nyongeza na huyu mwingine wa 120 ameihifadhi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24140/كيف-يتم-الجمع-بين-الاحاديث-المختلفة
  • Imechapishwa: 11/09/2024