Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema kuhusu Nabii Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا

”Ombeni msamaha kwa Mola wenu, hakika Yeye ni Mwingi mno wa kusamehe. Atakutumieni mvua nyingi ya kuendelea na atakuongezeeni mali na watoto na atakupeni mabustani na atakupeni mito.”[1]

Imekuja katika baadhi ya vitabu vya Hadiyth ya kwamba Ibn ´Abbaas ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayelazimiana na kuomba msamaha, basi Allaah atamfanyia kila huzuni njia ya faraja, kila dhiki njia ya kutoka na atamruzuku kupitia njia isiyoitarajia.”[2]

Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr ametaja katika ”at-Tamhiyd” Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayosema:

“Yeyote atakayesoma Suurah ”al-Waaqi´ah” kila siku basi hatopatwa na umasikini kabisa.”[3]

[1] 71:10-12

[2] Abu Daawuud (1518), Ibn Maajah (3819) na al-Haakim (4/262), aliyesema:

“Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Hakuipokea si al-Bukhaariy wala Muslim.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye na kusema:

“Katika cheni ya wapokezi yumo al-Hakam, ambaye hatambuliki.”

Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1518).

[3] Ibn-ul-Jawziy amesema:

“Ahmad bin Hanbal amesema kuwa Hadiyth ni dhaifu na inayopingana. Simtambui Shujaa´ wala as-Sariy.” (al-´Ilal al-Mutanaahiyah(1/105).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 299
  • Imechapishwa: 08/09/2025