Swali: Mvi katika mwili wote imekatazwa kung’olewa?
Jibu: Dhahiri katika Hadiyth ni kuenea, ndio. Nywele za ndevu na kichwa hubadilishwa kwa rangi ya manjano au nyekundu, si kwa rangi nyeusi.
Mwanafunzi: Katika mikono na miguu vivyo hivyo?
Ibn Baaz: Mikono haina nywele, kile ambacho kina nywele mtu anaenda kukiondoa, hakuna tatizo. Tunachozungumzia ni nywele za kichwa, nywele za ndevu na nywele za masharubu. Mikono na miguu si mahala pa nywele, lakini baadhi ya watu hutahiniwa kuwa na nywele.
Mwanafunzi: Je, kitendo hiki kinaonyesha kuwa ni dhambi kubwa?
Ibn Baaz: Dhahiri ni kuwa haya ni tishio, ndio. Kwa hiyo inapelekea kuwa ni dhambi kubwa, kwa sababu wametishiwa kuwa hawatanusa harufu ya Pepo. Hilo ni tisho.
Mwanafunzi: Je, hatofautishwi kati ya yule ambaye ndevu zake zote zimekuwa nyeupe kabisa na yule ambaye zina mchanganyiko wa weupe na weusi?
Ibn Baaz: Kadiri mvi zinavyokuwa nyingi, ndivyo kubadilisha rangi kunavyosisitizwa.
Mwanafunzi: Hii nyongeza inayosema:
“… na jiepukeni na rangi nyeusi.”
imesemwa kuwa ina kasoro?
Ibn Baaz: Baadhi yao wanaona kuwa imeingizwa tu. Lakini sahihi ni kuwa ni katika Hadiyth yenyewe na haikuingizwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31633/هل-النهي-عن-نتف-الشيب-يشمل-الجسد-كله
- Imechapishwa: 21/12/2025
Swali: Mvi katika mwili wote imekatazwa kung’olewa?
Jibu: Dhahiri katika Hadiyth ni kuenea, ndio. Nywele za ndevu na kichwa hubadilishwa kwa rangi ya manjano au nyekundu, si kwa rangi nyeusi.
Mwanafunzi: Katika mikono na miguu vivyo hivyo?
Ibn Baaz: Mikono haina nywele, kile ambacho kina nywele mtu anaenda kukiondoa, hakuna tatizo. Tunachozungumzia ni nywele za kichwa, nywele za ndevu na nywele za masharubu. Mikono na miguu si mahala pa nywele, lakini baadhi ya watu hutahiniwa kuwa na nywele.
Mwanafunzi: Je, kitendo hiki kinaonyesha kuwa ni dhambi kubwa?
Ibn Baaz: Dhahiri ni kuwa haya ni tishio, ndio. Kwa hiyo inapelekea kuwa ni dhambi kubwa, kwa sababu wametishiwa kuwa hawatanusa harufu ya Pepo. Hilo ni tisho.
Mwanafunzi: Je, hatofautishwi kati ya yule ambaye ndevu zake zote zimekuwa nyeupe kabisa na yule ambaye zina mchanganyiko wa weupe na weusi?
Ibn Baaz: Kadiri mvi zinavyokuwa nyingi, ndivyo kubadilisha rangi kunavyosisitizwa.
Mwanafunzi: Hii nyongeza inayosema:
“… na jiepukeni na rangi nyeusi.”
imesemwa kuwa ina kasoro?
Ibn Baaz: Baadhi yao wanaona kuwa imeingizwa tu. Lakini sahihi ni kuwa ni katika Hadiyth yenyewe na haikuingizwa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31633/هل-النهي-عن-نتف-الشيب-يشمل-الجسد-كله
Imechapishwa: 21/12/2025
https://firqatunnajia.com/nywele-ambazo-zinatakiwa-kubadilishwa-rangi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket