Nyusiku za Mtume katika kumi la mwisho

Swali: Akihuisha usiku wake[1], ina maana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akilala katika siku za kumi za mwisho?

Jibu: Ndio, hiyo ndio maana yake; ni kwamba alikuwa akihuisha usiku wake kwa kusoma Qur-aan, kuswali na kufanya du´aa.

[1] ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijitahidi katika zile nyusiku za mwisho za Ramadhaan kuliko anavyojitahidi katika nyusiku zengine.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25443/ما-معنى-احيا-ليله-في-الحديث
  • Imechapishwa: 21/03/2025