Nuuh ni Mtume wa kwanza baada ya kuzuka kwa shirki

Swali: Hadiyth iliyotangulia inasema kuwa Mtume wa kwanza ni Nuuh. Hata hivyo ipo Hadiyth nyingine inayosema kuwa ni Aadam.

Jibu: Nuuh ndiye Mtume wa kwanza kutumwa kwa watu wa ardhini baada ya kuzuka shirki ndani yake. Ni kama alivosema Aadam:

”Wewe ndiye Mtume wa kwanza ambaye Allaah amemtuma kwa watu wa ardhini.”

Kwa maana baada ya kujitokeza shirki. Kuhusu Aadam ni Mtume na Nabii kwa nisba yake mwenyewe na kizazi chake kabla ya kuzuka kwa shirki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24379/من-اول-الرسل-الى-اهل-الارض
  • Imechapishwa: 04/10/2024