Njia ya karibu na ya haraka zaidi kuinua hali duni ya waislamu

Swali: Tumeelewa kutoka kwa wanazuoni maana ya ustaarabu wa kweli na nguzo zake. Basi ni njia ipi iliyo karibu zaidi na ya haraka kwa kuinua hali duni ya waislamu kama alivyosema?

Jibu: Njia iliyo karibu zaidi, iliyo rahisi na yenye manufaa makubwa ni kushirikiana katika wema na uchaji Allaah, kueneza elimu yenye manufaa miongoni mwa watu katika vyuo, shule, kurekebisha mitaala ya elimu, kuwasogeza waalimu wema na kuwaweka mbali waovu. Haya yote ni katika kuandaa nguvu. Yote haya ni katika matendo mema. Matendo mema ni kueneza elimu yenye manufaa kati ya watu, kueneza mifumo yenye manufaa, kueneza shule zenye manufaa, vyuo vyenye manufaa na kusogeza waalimu wema na wengineo, kuwaweka mbali waovu na kuwa mkweli katika hilo kutoka kwa watawala, wanazuoni na wenye nafasi katika jamii na wanafunzi. Kukipatikana ukweli na uaminifu katika mambo haya yote, basi kheri kubwa itakuja haraka. Mambo haya yakiachwa na yasishughulikiwe, basi balaa litaendelea. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ

“Haukupateni katika msiba wowote basi ni kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono yenu na anasamehe mengi.”[1]

Misiba yetu ni kutokana na yale tuliyoyachuma. Tukirekebisha tuliyoharibu, tukirekebisha mifumo yetu, shule zetu, vyuo vyetu na tukishirikiana katika wema na uchaji Allaah pamoja na wakubwa wetu, wanazuoni wetu, mahakimu na wenye nafasi, mambo haya yakipatikana basi kheri nyingi itakuja, furaha itakuja na nusura yenye nguvu itakuja kwa idhini ya Allaah.

[1] 42:30

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1000/اقرب-طريق-للنهوض-بواقع-المسلمين
  • Imechapishwa: 05/01/2026