Njia mbili za kulipa Sunnah ya Fajr

Swali: Je, ni sahihi kwamba ulipaji wa sunnah ya Fajr una namna mbili; moja kwa moja baada ya swalah na baada y kuchomoza kwa jua na hili ndio bora zaidi?

Jibu: Sahihi inafuta neno bora zaidi. Nikimaanisha kuwa njia zote mbili zinafaa.

Swali: Ni ipi dalili ya hilo la pili ya kwamba aicheleweshe mpaka wakati wa kuchomoza kwa jua?

Jibu: Ipo Hadiyth ambapo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ambaye atapitwa na Sunnah ya Fajr, basi aiswali baada ya kuchomoza kwa jua.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (2361).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 167
  • Imechapishwa: 03/07/2022