Niwape nafasi wengine na nisihiji mara ya pili na mara ya tatu?

Swali 25: Baadhi ya watu wanashauri yule aliyeshahiji kwamba asihiji mara ya pili na ya tatu kwa hoja ya kwamba awape wengine nafasi. Ni upi mtazamo wako juu ya maneno haya?

Jibu: Mimi nasimama katika hili. Mara husema kwamba ikiwa tutaona msongamano mkali na kwamba mtu anajichosha nafsi yake katika jambo ambalo huenda kubaki kwake katika nchi yake kukawa ni unyenyekevu zaidi na kumcha zaidi Allaah, kwa sababu katika nchi yake atashughulika kumtaja Alllaah, kusoma Qur-aan, kufunga, kutoa swadaqah, kufanya wema na atatekeleza ´ibaadah akiwa na utulivu ndani yake, basi wakati mwingine husema kuwa hili ndio bora zaidi. Mara nyingine ikiwa ninapoona dalili juu ya kuhimiza Hajj na kubainisha ubora wake, husema kuwa Hajj ndio bora zaidi. Kisha ikiwa nitaona pia kwamba wenye kuhiji baadhi yao wanahiji faradhi na baadhi yao Hajj ya kujitolea na hakuna shaka kwamba maeneo ya ´ibaadah kwa yule anayetekeleza faradhi yana haki zaidi, kwa sababu wao wana haki zaidi nayo kuliko yule anayehiji Hajj ya kujitolea. Mimi niko katika kusitasita katika hili. Naogopa ikiwa nitawakataza wasihiji ilihali Maandiko yamekuja yakihimiza Hajj, kwamba katika hilo kutakuwa na dhambi kubwa. Ikiwa nitaangalia madhara na kupunguza madhara juu ya watu, husema kutohiji ndio bora zaidi. Mwenye kuwa na ziada ya mali, basi milango ya kheri ni mingi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/33-34)
  • Imechapishwa: 26/05/2026