Swali 27: Je, yule anayewakilishwa kuhiji kwa niaba ya mtu mwingine anapata kile alichosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayehiji na asifanye upuuzi wala kufanya ufuska, basi atarudi kutoka kwenye madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”[1]?
Jibu: Jibu linategemea juu ya swali hili, je, mtu huyu amehiji kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya mwingine? Hakika amehiji kwa ajili ya mwingine na hakuhiji kwa ajili ya nafsi yake. Hivyo hapati ujira ule aliousema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu hakika amefanya Hajj kwa ajili ya mwingine. Lakini – kwa idhini ya Allaah – ikiwa amekusudia kumnufaisha ndugu yake na kutimiza haja yake, basi Allaah (Ta´ala) atamlipa thawabu.
[1] al-Bukhaariy (1521) na Muslim (1350).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/34)
- Imechapishwa: 26/05/2026
Swali 27: Je, yule anayewakilishwa kuhiji kwa niaba ya mtu mwingine anapata kile alichosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayehiji na asifanye upuuzi wala kufanya ufuska, basi atarudi kutoka kwenye madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”[1]?
Jibu: Jibu linategemea juu ya swali hili, je, mtu huyu amehiji kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya mwingine? Hakika amehiji kwa ajili ya mwingine na hakuhiji kwa ajili ya nafsi yake. Hivyo hapati ujira ule aliousema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu hakika amefanya Hajj kwa ajili ya mwingine. Lakini – kwa idhini ya Allaah – ikiwa amekusudia kumnufaisha ndugu yake na kutimiza haja yake, basi Allaah (Ta´ala) atamlipa thawabu.
[1] al-Bukhaariy (1521) na Muslim (1350).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/34)
Imechapishwa: 26/05/2026
https://firqatunnajia.com/malipo-na-fadhilah-zinaenda-kwa-yule-anayehijiwa/