Niswali katika msikiti upi kati ya misikiti miwili hii?

Swali: Je, ni bora kuswali katika msikiti mkuu au msikiti ambao utamfanya kupiga hatua nyingi?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Watu wenye ujira mwingi katika swalah ni wale wenye kutembea kutokea sehemu za mbali.”

”Swalah ya mtu na mtu mwingine ni takasifu zaidi kuliko swalah yake peke yake, pamoja na watu wawili ni takasifu zaidi kuliko swalah yake pamoja na mtu mmoja, na kadiri watavyokuwa wengi zaidi ndio inapendeza zaidi kwa Allaah.”

Kila ambavo msikiti utakuwa mbali zaidi ndio bora.

Swali: Hata kama si msikiti mkuu?

Jibu: Hata kama si msikiti mkuu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar Ahaadiyth-is-Swiyaam, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 18/11/2024