Swali: Vipi ngamia mchanga aliyepotea?

Jibu: Ikiwa anachelea juu yake kutokana na wanyama wakali, kama vile mbwa mwitu, amchukue na amtangaze kwa kujengea kipimo juu ya kondoo na mbuzi, kwa sababu ni mdogo na hawezi kustahamili dhoruba.

Swali: Baadhi ya watu wanamchukua kwa ajili yao wenyewe na kusema kwamba badala achukuliwe na mwingine basi yeye anamchukua.

Jibu: Inafaa kumchukua kwa nia ya uaminifu. Hata hivyo haijuzu kumchukua kwa nia ya kumtamani. Ima amchukue kwa nia ya uaminifu na asimamie yale yanayompasa au amwache na asimchukue. Ikiwa ni mnyonge basi anapaswa kumchukua ili amtangaze au amwache mahali pake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24172/حكم-ضالة-صغار-الابل
  • Imechapishwa: 12/09/2024