Swali: Ni vipi tutatatua tatizo hili; wako wasichana wengi ambao wanataka kuolewa. Lakini hata hivyo hawajajiwa na kijana yoyote kwa sababu ya mahari kuwa makubwa. Baadhi ya maimamu wa misikiti wameshtakiwa kubaki kwa wasichana wao pasi na kuolewa kwa sababu ya ukubwa wa mahari.

Jibu: Naamini kwamba kutatua jambo hili ni rahisi; anapokuja kijana na ikiwa baba anataka kumuozesha msichana wake amwambia: “Nipe unachotaka.” Tumefikiwa na khabari kwamba kuna watu waliowafikishwa ambao waposaji  wamewapa yale mahari walioleta. Hili pasi na shaka ni jambo lenye kheri. Ni kheri iliokubwa kabisa. Huku ni kuwafanyia vizuri wasichana wao na ni kuwafanyia vizuri vilevile wale wanaokuja kuposa.

Namna ya kutatua tatizo hili ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kuwawafikisha watu/wazee kutoka katika kabila lao au wasiotoka katika kabila lao na wawatangazie kuwa wawaozeshe kwa mahari mepesi. Mimi naamini kwamba wakifanya hivo basi watajiwa na waposaji wengi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1058
  • Imechapishwa: 21/03/2019