Nini makusudio ya hajj yenye kukubaliwa?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hajj yenye kukubaliwa aina malipo mengine isipokuwa Pepo.”

Ni ipi hajj yenye kukubaliwa?

Jibu: Hajj yenye kukubaliwa ni ile aliyoitekeleza kwa mujibu wa Sunnah na kwa ajili ya Allaah pekee. Ni ile hajj iliyotimiza masharti haya mawili:

1 – Iwe ameifanya kwa ajili ya Allaah pekee.

2 – Iwe ni yenye kuafikiana na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/02-02.mp3
  • Imechapishwa: 20/11/2017