Swali: Ni nini maana ya neno mnafiki? Ni nani mtu Faasiq na Faajir?

Jibu: Mnafiki ni yule mtu ambaye anadhihirisha kheri na anaficha shari. Ikiwa anadhihirisha Uislamu na anaficha kufuru ni unafiki wa I´tiqaad ambao ni unafiki mkubwa. Na ikiwa anadhihirisha ´ibaadah na kupenda kheri na anaficha yasiyokuwa hayo ni unafiki mdogo ambao ni unafiki wa kimatendo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Alama za mnafiki ni tatu; akizungumza anasema uongo, akiahidi hatimizi na akiaminiwa anafanya khiyana.”

Haya yanapitika kwa muislamu. Lakini hata hivyo ni miongoni mwa sifa za wanafiki na ni jambo linalopunguza imani.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15208
  • Imechapishwa: 28/06/2020