Nini cha kufanya makaratasi mengi yenye jina la Allaah?

Swali: Karatasi zilizo na Basmalah zinapaswa kutupwa kwenye takataka au zinafanywa nini kwa sababu ni nyingi?

Jibu: Lifutwe na kuchanwa jina la Allaah au liteketezwe kikamilifu na inatosha kufanya hivo.

Swali: Vipi ikiwa litafutwa kwa kitu?

Jibu: Likifutwa inatosha.

Swali: Vipi kuhusu magazeti?

Jibu: Magazeti yahifadhiwe. Hapana neno akayahifadhi kwenye kabati au mahali pengine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22889/حكم-الاوراق-المهملة-التي-عليها-البسملة
  • Imechapishwa: 28/05/2025