Nini anachosema anayefarijiwa kwa msiba?

Swali: Ni ipi Sunnah pale mtu aliyepata msiba anapoambiwa:

إن لله ما أخذ، و (لله) ما أعطي، وكل شئ عنده إلى أجل مسمى فالتصبر، ولتحتسب

”Hakika ni Chake Allaah kile alichokichukua na ni Chake Allaah alichotoa na kila kitu Kwake kina muda uliopangwa. Basi afanye subira na atarajie malipo kutoka Kwake.”?

Je, anayefarikiwa au aliyepata msiba anapaswa kumjibu nini anayempa pole?

Jibu: Aseme chochote chema kinachofaa. Hakuna maneno maalum yaliyowekewa mipaka. Akiambiwa:

أحسن الله عزاءك

”Allaah akufanyie wema msiba wako.”

au:

إن لله ما أخذ، و (لله) ما أعطي، وكل شئ عنده إلى أجل مسمى فالتصبر، ولتحتسب

”Hakika ni Chake Allaah kile alichokichukua na ni Chake Allaah alichotoa na kila kitu Kwake kina muda uliopangwa. Basi afanye subira na atarajie malipo kutoka Kwake.”

Yeye ajibu kwa kusema:

”Namuomba Allaah anisaidie, namwomba Allaah aniwafikishe na kwamba namshukuru Allaah kwa kila hali au maneno yoyote mazuri yanayofaa.”

Kwa kifupi ni kwamba hakuna chochote kilichowekewa mpaka. Hatutambui kuwepo chochote kilichowekewa mpaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1029/كيفية-اجابة-المعزين
  • Imechapishwa: 09/01/2026