Nini anachofanya aliyeswali vibaya?

Swali: Vipi mtu akiswali na akafanya vibaya katika swalah yake kwa ujinga?

Jibu: Ikiwa ni makosa yanayoiharibu basi airudie na ikiwa sio makosa yanayoiharibu atafunzwa na hatoirudia. Ikiwa makosa yanahusiana na nguzo, kama vile utulivu na mengineyo, afunzwe na kuirudia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha bwana mmoja kuirudia swalah yake. Na ikiwa amefanya upungufu katika baadhi ya mambo katika yanayopendeza ambayo hayaiharibu, haidhuru. Lakini afunzwe njia kamilifu na wala haidhuru.

Swali: Vipi ikiwa amefanya makosa katika nguzo moja tu?

Jibu: Afunzwe na airudie.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24239/ماذا-يفعل-من-اساء-في-صلاته-جاهلا
  • Imechapishwa: 16/09/2024