Swali: Je, inatakiwa kumfahamisha mtu anapewa zakaah ya kwamba pesa hii ni zakaah?

Jibu: Ikiwa anachelea ya kwamba ni tajiri. Ikiwa kuna sintofahamu. Lakini ikiwa unajua kuwa yeye ni maskini, basi huna haja ya kumwambia kitu.

Swali: Ninajua kuwa yeye ni maskini, lakini kwa mfano ni ndugu yangu wa karibu?

Jibu: Umpe na usimwambie kitu. Lakini ikiwa una shaka naye, labda ana pesa na wewe hujui, basi mweleze kuwa pesa hiyo ni ya zakaah.

Swali: Najua kuwa yeye hana pesa, lakini baadhi yao wanajizuia kuchukua zakaah?

Jibu: Hapana, hapana, mpe wala usimwambie kuwa ni zakaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24657/هل-يلزم-اخبار-من-تدفع-اليه-الزكاة-بانها-زكاة
  • Imechapishwa: 22/11/2024