Swali: Mama yangu amefariki na hakumuusia mtu yeyote kuhiji kwa niaba yake. Je, inajuzu mimi kuhiji kwa niaba ya mama yangu?

Jibu: Ndio, ikiwa hakuhiji, basi wahiji kwa niaba yake hijjah ya faradhi. Ikiwa tayari alishahiji, basi hiyo itakuwa ni hijjah ya kujitolea. Allaah akulipe kheri. Hili ni miongoni mwa aina muhimu zaidi za kuwafanyia wema wazazi. Mmesikia Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa na mtu:

”Je, kunabaki kitu cha kuwafanyia wema wazazi wangu baada ya kufariki kwao?” Akasema: ”Ndio, kuwaombea du´aa, kuwaombea msamaha, kutekeleza maagano yao baada yao, kuwakarimu marafiki zao na kuwaunga ndugu ambao haungwi isipokuwa kupitia wao.”

Kwa hiyo kuhiji kwa niaba yao ni miongoni mwa matendo bora zaidi na kutekeleza wasia wao – ikiwa wasia huo haupingani na Shari´ah – kuwaombea du´aa, swalah ya jeneza na kuwaombea msamaha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1357/هل-الحج-عن-الوالدة-جاىز
  • Imechapishwa: 14/12/2025