Nimemchumbia mwanamke mwenye dini lakini mama yangu hamtaki

Swali: Nimemchumbia msichana anayeswali, anayefunga na anayelinda faradhi, lakini mama yangu hataki awe mke wangu kwa sababu ya tofauti zilizopo kati ya familia zao na ameng´ang´ania juu ya jambo hilo. Je, nimtii mama yangu au nifanye nini?

Jibu: Usiharakishe kumtii mama yako katika jambo hili. Utii unakuwa katika mema yaliyo halali, si katika maasi. Ndoa ni jambo muhimu sana. Ikiwa huyo mwanamke ni mwema katika dini yake na yuko katika msimamo mzuri, basi inakupasa uzungumze na mama yako kwa mtindo mzuri na kwa maneno laini na mazuri ili aridhike – Allaah akitaka.

Vilevile inakupasa umnasihi huyo mwanamke awe na tabia njema, aonyeshe mwenendo mzuri na maadili mema mbele ya mama yako ili kusiwepo chuki au uhasama kati yake na watu wa familia yako.

Kwa kifupi ni kwamba wewe uko katika nafasi nyeti miongoni mwa nguzo za Uislamu. Kwa hivyo ni wajibu wako kujitahidi kumridhisha mama yako na kuwaridhisha waliokuzunguka kwa maneno mazuri na mtindo mzuri. Pia umnasihi mke mtarajiwa atumie upole na maneno mema katika kushughulika nao ili – kwa idhini ya Allaah – patokee maelewano, umoja na kuepusha kufikia talaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2189/حكم-من-خطب-بنتا-ذات-دين-مع-كون-الام-ترفضها
  • Imechapishwa: 05/06/2026