Swali: Ikiwa kuna kuhifadhi bidhaa katika nyakati ambazo watu hawana uhitaji wa dharurah wa bidhaa hizo, lakini muuzaji anatarajia bei kupanda. Je, hilo linajuzu?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hapana anayehifadhi bidhaa isipokuwa mkosefu.”
Anayehifadhi bidhaa basi amekosea. Hii inaonesha kuwa kuhifadhi bidhaa ni haramu. Hata hivyo wanazuoni wameeleza kuwa kuhifadhi bidhaa kunakokatazwa ni kule kunaofanyika katika nyakati ambazo watu wanapata mashaka, kama chakula kuwa ghali, kisha mtu akinunua ili auze kwa bei ya juu zaidi, hili halijuzu kwa sababu linawaumiza watu. Ama katika nyakati za wasaa, neema kuwa nyingi na bidhaa kupatikana kwa wingi na kununua huko hakusababishi dhiki kwa watu wala kupandisha bei sokoni, basi mtu akinunua kitu na akakiweka ili akiuze baadaye kwa faida, hili ni jambo la biashara, na haliitwi kuhifadhi bidhaa. Vivyo hivyo ikiwa mtu amenunua mazao kutoka kwa mkulima, kama nafaka au tende, kisha akayahifadhi hadi wakati anaotarajia bei itakuwa bora zaidi, kwa kuwa kwa sasa soko ni dhaifu na bei ni ya chini, basi kuhifadhi mazao yake hadi wakati mwingine hakuhesabiwi kuwa ni kuhifadhi bidhaa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2140/حكم-من-احتكر-سلعة-ليس-في-احتكارها-مشقة-على-الناس
- Imechapishwa: 05/06/2026
Swali: Ikiwa kuna kuhifadhi bidhaa katika nyakati ambazo watu hawana uhitaji wa dharurah wa bidhaa hizo, lakini muuzaji anatarajia bei kupanda. Je, hilo linajuzu?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hapana anayehifadhi bidhaa isipokuwa mkosefu.”
Anayehifadhi bidhaa basi amekosea. Hii inaonesha kuwa kuhifadhi bidhaa ni haramu. Hata hivyo wanazuoni wameeleza kuwa kuhifadhi bidhaa kunakokatazwa ni kule kunaofanyika katika nyakati ambazo watu wanapata mashaka, kama chakula kuwa ghali, kisha mtu akinunua ili auze kwa bei ya juu zaidi, hili halijuzu kwa sababu linawaumiza watu. Ama katika nyakati za wasaa, neema kuwa nyingi na bidhaa kupatikana kwa wingi na kununua huko hakusababishi dhiki kwa watu wala kupandisha bei sokoni, basi mtu akinunua kitu na akakiweka ili akiuze baadaye kwa faida, hili ni jambo la biashara, na haliitwi kuhifadhi bidhaa. Vivyo hivyo ikiwa mtu amenunua mazao kutoka kwa mkulima, kama nafaka au tende, kisha akayahifadhi hadi wakati anaotarajia bei itakuwa bora zaidi, kwa kuwa kwa sasa soko ni dhaifu na bei ni ya chini, basi kuhifadhi mazao yake hadi wakati mwingine hakuhesabiwi kuwa ni kuhifadhi bidhaa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2140/حكم-من-احتكر-سلعة-ليس-في-احتكارها-مشقة-على-الناس
Imechapishwa: 05/06/2026
https://firqatunnajia.com/hali-mbalimbali-za-kuhifadhi-bidhaa-na-hukumu-zake/