Swali: Nimemuona maiti amewekwa Qur-aan juu ya kifua chake. Je, hilo linajuzu au halijuzu?

Jibu: Hapana, haikusuniwa kuweka Qur-aan juu ya maiti. Lakini baadhi ya watu wamesikia kuwa maiti huwekewa kitu fulani juu yake na wakafikiri kuwa Qur-aan ndio bora zaidi kuwekwa. Lengo halikuwa kuweka Qur-aan. Lengo ni kuweka kitu chenye uzito juu ya tumbo lake ili asivimbe kabla hajaoshwa na kupelekwa makaburini. Hivyo huwekwa chuma, jiwe au mfano wa hivyo miongoni mwa vitu vizito juu ya tumbo lake mpaka aoshwe, kwa sababu huenda akavimba. Kwa hiyo huwekwa kitu chenye uzito kinachofaa ili kuzuia kuvimba mpaka aoshwe na amalizane na maziko.

Msahafu si chombo cha kutia uzito. Msahafu umeandikwa na kuchapishwa ili usomwe na kunufaika nao. Kwa hiyo hauwekwi juu ya maiti. Bali huwekwa kitu chenye uzito kama mbao, chuma au jiwe juu ya tumbo. Haya yamesemwa na baadhi ya wanazuoni. Wamesema kuwa kufanya hivo hupunguza kuvimba. Jambo hili ni jepesi. Lakini msahafu hauwekwi juu ya maiti.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1969/حكم-وضع-القران-على-صدر-الميت-قبل-تغسيله
  • Imechapishwa: 05/06/2026