Swali: Ni ipi hukumu ya kulaani dini ya mtu?

Jibu: Kulaani dini, ikiwa anakusudia dini ya Kiislamu, basi hilo ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Ama ikiwa anakusudia uyahudi, dini ya kuabudia mizimu au dini ya kuabudia moto, basi hilo si hivyo. Lakini kulaani dini ya muislamu – na dini ya muislamu ni Uislamu – hili ni kuritadi.

Inapaswa kutanabahishwa juu ya jambo hili na watu waonywe dhidi yake. Mwenye kufanya hivo atiwe adabu, kwa sababu anastahiki kuadabishwa kwa tendo hili baya.

Swali: Je, lina kafara?

Jibu: Ni kutubu kwa Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1814/حكم-لعن-دين-الشخص
  • Imechapishwa: 05/06/2026