Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth kuhusu kuadhini na kukimu kwenye masikio ya mtoto mchanga?
Jibu: Yametajwa katika Hadiyth aliyoipokea at-Tirmidhiy na wengineo. Hata hivyo katika cheni yake ya wapokezi kuna udhaifu. Hata hivyo wameifanyia kazi wanazuoni kadhaa, kama ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz na wengine. Pia limetajwa katika Hadiyth nyingine inayoiunga mkono ambayo nayo ni dhaifu. Kwa hiyo anayefanya hakuna tatizo. Hadiyth zimekuja kutiana nguvu, japokuwa ndani yake kuna udhaifu. Lakini zinapeana nguvu. Waislamu wengi wameifanyia kazi. Anayeaacha ni sawa.
Swali: Hili hufanywa lini?
Jibu: Hufanywa siku ya saba au siku ya kwanza. Huadhiniwa katika sikio la kulia na hukimiwa katika sikio la kushoto. Humpa jina siku ya kwanza au siku ya saba na hunyoa kichwa chake. Yote haya ni Sunnah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1901/درجة-الحديث-الوارد-في-الاذان-والاقامة-في-اذني-المولود
- Imechapishwa: 05/06/2026
Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth kuhusu kuadhini na kukimu kwenye masikio ya mtoto mchanga?
Jibu: Yametajwa katika Hadiyth aliyoipokea at-Tirmidhiy na wengineo. Hata hivyo katika cheni yake ya wapokezi kuna udhaifu. Hata hivyo wameifanyia kazi wanazuoni kadhaa, kama ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz na wengine. Pia limetajwa katika Hadiyth nyingine inayoiunga mkono ambayo nayo ni dhaifu. Kwa hiyo anayefanya hakuna tatizo. Hadiyth zimekuja kutiana nguvu, japokuwa ndani yake kuna udhaifu. Lakini zinapeana nguvu. Waislamu wengi wameifanyia kazi. Anayeaacha ni sawa.
Swali: Hili hufanywa lini?
Jibu: Hufanywa siku ya saba au siku ya kwanza. Huadhiniwa katika sikio la kulia na hukimiwa katika sikio la kushoto. Humpa jina siku ya kwanza au siku ya saba na hunyoa kichwa chake. Yote haya ni Sunnah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1901/درجة-الحديث-الوارد-في-الاذان-والاقامة-في-اذني-المولود
Imechapishwa: 05/06/2026
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-usahihi-wa-hadiyth-ya-kuadhini-na-kukimu-kwenye-masikio-ya-mtoto-mchanga/