Hakuswali kwa sababu ya theluji na baridi kali

Swali: Niliacha swalah kwa kipindi cha wiki tatu kwa kwa kushindwa kutawadha kwa sababu ya baridi kali na theluthi. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni kosa na ujinga. Ni wajibu kwako kuswali vile unavyoweza. Kama umeshindwa kutawadha kwa sababu ya baridi kali na theluji, basi unaweza daima kufanya Tayammum. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

“Mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akija kutoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ardhi yote imefanywa kwangu kuwa ni sehemu ya kuswalia na yenye kujitwahirisha kwayo. Kwa hivyo mtu yeyote katika ummah wangu ambaye swalah itamkuta popote basi aswali hapo.”[2]

Unapoingia wakati wa swalah basi unalazimika kuswali. Ikiwa unaweza kutawadha basi ndio inavotakikana. Vinginevyo unapaswa kutumia udongo. Ni wajibu kwako kutubia kwa Allaah (´Azza wa Jall) kikweli na uziswali swalah zilizokupita.

[1] 5:6

[2] al-Bukhaariy na Muslim

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/94-95)
  • Imechapishwa: 04/06/2026