Swali: Ni ipi hukumu ya matibabu ya kunyoosha meno?
Jibu: Kunyoosha meno kumegawanyika sampuli mbili:
1 – Kufanya hivo kwa ajili kuzidisha urembo. Ni haramu na haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kufanya chanjo na mwanamke mwenye kufanywa chanjo, mwanamke mwenye kuchonga nyusi na mwanamke mwenye kuchongwa nyusi na mwanamke mwenye kufanya mwanya kwa ajili ya kutafuta urembo wanaoyabadilisha maumbile ya Allaah.”[1]
Mambo ni namna hii licha ya kwamba mwanamke anatakiwa kujipamba na ni mwenye kukulia juu ya kujipamba. Ikiwa ni haramu kwa wanawake basi wanaume ni aula zaidi.
2 – Ikiwa kuyarekebisha ni kwa ajili ya kuondoa kasoro, basi hapana vibaya. Baadhi ya watu wanaweza kuwa na meno yasiyopangika vibaya kwa namna ya kwamba yanaonekana vibaya. Katika hali hii ni sawa kwa mtu kuyarekebisha. Kwa sababu kufanya hivo ni kwa ajili ya kuondoa kasoro na sio kuzidisha kasoro. ´Arajah bin As´ad (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Pua yangu ilikatwa siku ya Kulaab kabla kipindi kabla ya kuja Uislamu. Hivyo nikachukua pua bandia ya dhahabu. Baada ya kuoza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaniamrisha kuweka pua ya dhahabu.”[2]
Lengo ilikuwa kuondoa kasoro na sio kwa ajili ya kuzidisha urembo.
[1] al-Bukhaariy (5943) na Muslim (2125).
[2] Ahmad (5/23), Abu Daawuud (4232) na at-Tirmidhiy (1770) aliyesema:
”Hadiyth ni nzuri na geni.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/22-23)
- Imechapishwa: 04/06/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya matibabu ya kunyoosha meno?
Jibu: Kunyoosha meno kumegawanyika sampuli mbili:
1 – Kufanya hivo kwa ajili kuzidisha urembo. Ni haramu na haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kufanya chanjo na mwanamke mwenye kufanywa chanjo, mwanamke mwenye kuchonga nyusi na mwanamke mwenye kuchongwa nyusi na mwanamke mwenye kufanya mwanya kwa ajili ya kutafuta urembo wanaoyabadilisha maumbile ya Allaah.”[1]
Mambo ni namna hii licha ya kwamba mwanamke anatakiwa kujipamba na ni mwenye kukulia juu ya kujipamba. Ikiwa ni haramu kwa wanawake basi wanaume ni aula zaidi.
2 – Ikiwa kuyarekebisha ni kwa ajili ya kuondoa kasoro, basi hapana vibaya. Baadhi ya watu wanaweza kuwa na meno yasiyopangika vibaya kwa namna ya kwamba yanaonekana vibaya. Katika hali hii ni sawa kwa mtu kuyarekebisha. Kwa sababu kufanya hivo ni kwa ajili ya kuondoa kasoro na sio kuzidisha kasoro. ´Arajah bin As´ad (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Pua yangu ilikatwa siku ya Kulaab kabla kipindi kabla ya kuja Uislamu. Hivyo nikachukua pua bandia ya dhahabu. Baada ya kuoza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaniamrisha kuweka pua ya dhahabu.”[2]
Lengo ilikuwa kuondoa kasoro na sio kwa ajili ya kuzidisha urembo.
[1] al-Bukhaariy (5943) na Muslim (2125).
[2] Ahmad (5/23), Abu Daawuud (4232) na at-Tirmidhiy (1770) aliyesema:
”Hadiyth ni nzuri na geni.”
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/22-23)
Imechapishwa: 04/06/2026
https://firqatunnajia.com/matibabu-ya-waya-kwenye-meno/