51. Kumwomba Allaah akuongoze katika njia ilionyooka katika kila Rak´ah

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

صِرَاطَ الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ

”… njia ya wale uliyowaneemeshe.”[1]

Njia ya wale uliyowaneemeshe. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَن يُطِعِ اللّهَ وَالرَّسُولَ فَأُوْلَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاء وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا

“Atakayemtii Allaah na Mtume basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha – Manabii na wakweli na mashahidi na waja wema – na uzuri ulioje kuwa na tangamano kama hili!”[2]

غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ

”… si ya wale Uliowaghadhibikia… ”

Walioghadhibikiwa nao ni mayahudi waliopewa elimu pasi na kuitendea kazi. Tunamuomba Allaah atukinge na njia yao.

وَلاَ الضَّالِّينَ

”… na wala wale waliopotea!”

Waliopotea nao ni manaswara wanaomuabudu Allaah kwa ujinga na upotevu. Tunamuomba Allaah atukinge na njia zao. Dalili ya waliopotea ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

“Sema: “Je, Tukujulisheni ni wepi ambao matendo yao yamekhasirika? Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia nao wakidhani kwamba wanatenda vizuri.”[3]

Kadhalika amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika mtafuata nyenendo za waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na pima kwa pima hata wakiingia katika shimo la mburukenge mutaingia nao.” Wakauliza: “Je, unakusudia mayahudi na manasara?” Akasema: “Ni nani wengine ikiwa si wao?”[4]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hadiyth nyingine inasema:

“Wamegawanyika mayahudi katika mapote sabini na moja, wakagawanyika manaswara katika mapote sabini na mbili na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu – yote hayo yataingia Motoni ila moja tu.” Maswahabah wakauliza: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litalokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi na Maswahabah zangu.”[5]

MAELEZO

Njia ilionyooka ambayo muislamu humuomba Mola wake amwongoze juu yake ni njia ya walioneemeshwa miongoni mwa Mitume, wakweli, mashahidi na waja wema. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo mpate kumcha.”[6]

Yeye humuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika kila Rak´ah ya Rak´ah za swalah yake amuongoze njia ya haki na uongofu. Sambamba na hilo anamwomba amuepushe na njia ya watu wa upotofu na upotevu miongoni mwa mayahudi na manaswara. Imekuja katika Hadiyth:

“Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu… ”

Ameipokea al-Bukhaariy (7320) na Muslim (2669) kupitia kwa Abu Sa´iyd. Sehemu yake ya mwanzo imekuja kwa al-Bukhaariy kwa tamko lisemalo:

“Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri, pima kwa pima… “

Imekuja kwa Muslim:

“Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na pima kwa pima… “

Hadiyth ya kufarikiana kwa ummah imepokewa kutoka kwa kundi la Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Angalia uchambuzi wake katika maelezo ya Hadiyth nambari (16937) katika ”Musnad” ya Imaam Ahmad. Aidha tazama ”as-Silsilah as-Swahiyhah”, uk. 203-204 ya al-Albaaniy. Kumenakiliwa usahihi wake kutoka kwa Ibn Taymiyyah, ash-Shaatwibiy na al-´Iraaqiy. Maana ya ummah iliyotajwa katika Hadiyth ni ummah ulioitikia (أمة الإجابة). Makundi haya sabini na tatu ni waislamu: kundi moja ni la waliookoka, nao ni wale waliokuwa juu ya alichokuwa nacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake, makundi sabini na mawili wamepewa makemeo ya Moto kwa sababu ya kupotoka kwao kutoka njia ya haki, jambo lao ni kwa Allaah kwa maana ya kwamba akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe.

Kuhusu ummah unaolinganiwa (أما أمة الدعوة) ni kila mtu na jini tangu alipotumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hadi kisimame Qiyaamah. Humo wanaingia pia mayahudi, manaswara na kila aina ya dini ya kikafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake. Hatosikia kuhusu mimi, ni mamoja awe myahudi au mkristo, kisha akafa na asiamini yale niliyotumwa kwayo isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.”

Ameipokea Muslim (386) kupitia kwa Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh). Tazama ”Fataawaa” za Shaykh-ul-Islaam (7/218) na ”Fataawaa” za al-Lajnah ad-Daa’imah (2/157).

[1] 01:07

[2] 04:69

[3] 18:103-104

[4] al-Bukhaariy (4356) na Muslim (2669).

[5] Ibn Maajah (3992), at-Tirmidhiy (2641) na Abu Daawuud (4596). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (171).

[6] 6:153

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 58-61
  • Imechapishwa: 04/06/2026