Nikubali zawadi ya anayefanya kazi benki?

Swali: Je, inakubaliwa zawadi ya anayeshughulika na ribaa?

Jibu: Ndiyo, ikiwa mali yake yote haitokani na ribaa. Allaah ameturuhusu kula chakula cha mayahudi ilihali wanajihusisha na ulaji ribaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinunua chakula kutoka kwao na kuweka rehani ngao yake. Lakini ikiwa unajua kuwa zawadi hiyo inatokana na mali ya ribaa au mali yake yote ni ya ribaa, basi usiipokee.

Swali: Yeye anafanya kazi benki na hana chanzo kingine cha mapato isipokuwa hiyo benki?

Jibu: Usikubali zawadi yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25384/هل-تقبل-هدية-من-يتعامل-بالربا
  • Imechapishwa: 08/03/2025