Swali: Nikimuona mtu anazini na mimi niko mwenyewe sina mashahidi wanne nifiche jambo hilo au nifanye nini?

Jibu: Ndio, kama tulivyotangulia kusema lifiche na umnasihi. Kwa mfano ikiwa ni mwanamke anayejulikana kwa uzinzi unaweza kwenda kwa mume wake na kumshauri atengane naye. Au ikiwa ni mwanamke anayetambulika kwa uzinzi unaweza kuwashauri watu wasimwache akaingia katika nyumba zao. Usitamke waziwazi. Ukisema waziwazi basi wewe mwenyewe ndiye ambaye utasimamishiwa adhabu.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 247-248
  • Imechapishwa: 10/03/2025