Nibadilishe jina la ´Abdul-Mu´twiy nililopewa na baba yangu?

Swali: Ikiwa baba yangu alinipa jina ´Abdul-Mu´twiy na wanazuoni wa leo miongoni mwao wapo wanaokataa majina isipokuwa yale yaliyotajwa ndani ya Qur-aan miongoni mwa majina ya Allaah (Ta´ala). Je, ni wajibu kwangu kulibadilisha jina langu liwe ´Abdul-Qudduus au jina jingine?

Jibu: Hapana, al-Mu´twiy ni miongoni mwa majina ya Allaah. Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim kupitia kwa Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mimi ni mgawaji tu na Allaah ndiye Mtoaji.”

Kwa hiyo jina ´Abdul-Mu´twiy halina tatizo. Ni jina linalojuzu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1523/حكم-التسمي-بـ-عبد-المعطي
  • Imechapishwa: 27/03/2026