Ni yepi yaliyopendekezwa katika I´tikaaf?

Swali: Ni mapendekezo yepi ya I´tikaaf?

Jibu: Imependekezwa kwa mtu kujishughulisha na kumtii Allaah (´Azza wa Jall) katika kusoma Qur-aan, kuleta Adhkaar, kuswali na mengineyo. Asipoteze muda wake katika yasiyokuwa na faida kama wanavyofanya baadhi ya wafanyao I´tikaaf. Utawaona wanabaki msikitini na kila wakati wanajiwa na watu wanaomzungumzisha na wanakata I´tikaaf zao bila ya faida yoyote. Ama kuzungumza wakati fulani pamoja na baadhi ya watu na baadhi ya familia hakuna neno. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na ya Muslim ambapo Hafswah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alimwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akazungumza nae kiasi cha saa moja kisha akaondoka zake kwenda nyumbani kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/175)
  • Imechapishwa: 21/06/2017