Ni wategemezi wa watu, na sio Allaah

Swali: Vipi kuhusu watu ambao wanashinda msikitini na kudai kwamba wao wanamtegemea Allaah na wala hawafanyi sababu zozote, wakajibiwa kwamba wao ni wenye kuwategemea watu.

Jibu: Amepatia. Ni kama ilivyopokelewa kuhusu wasafiri waliofika kutoka Yemen na hawakuja na akiba yoyote. Wamekuja mikono mitupu wakiwaomba watu. Walipoambiwa wakasema kuwa eti wanamtegemea Allaah, ambapo baadhi ya Maswahabah wakawaambia kuwa ni walaji. Hali ni hiyohiyo. Yule ambaye anaacha kufanya sababu sio mtegemezi. Hakuna anachofanya isipokuwa kuwabebesha watu mizigo yake ili aweze kuwaomba na kuwaudhi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24338/حكم-من-يترك-الاسباب-بزعم-التوكل
  • Imechapishwa: 01/10/2024